BURUDANI

Andy Ruiz Junior Atwaa Taji La Ubondia Wa Dunia Baada Ya Kumtwangwa Anthony Joshua!

on

Kutoka kwenye pambano la ngumi,Bondia wa uzani mzito Andy Ruiz Jr ameushangaza ulimwengu kwa kumshinda bingwa wa ndondi katika uzani huo Anthony Joshua.

Joshua ambaye amepigiwa upatu kumrithi bingwa wa zamani katika uzani huo Mohamed Ali aliangushwa mara nne kabla ya refa kuingilia kati na kusitisha pigano hilo kunako raundi ya saba.

Andy Ruiz Jr aliushangaza ulimwengu katika historia ya ndondi na kufanikiwa kushinda mataji ya IBF, WBO na WBA yaliokuwa yakimilikwa na Anthony Joshua.

Katika pigano lililovutia wengi katika ukumbi maarufu wa ndondi nchini Marekani Mew York Madison Square Garden, Ruiz alionekana yupo vizuri zaidi ya Joshua toka awali kwa kumzidi nguvu na maarifa.

Joshua alipigiwa upatu kushinda pigano hilo na wengi kwa urahisi huku wachanganuzi wakifananisha kilichompata bondia huyo sawa na waliyoyapitia mabingwa wa zamani Lennox Lewis na Mike Tyson ambao pia waliwahi kupigwa na wapinzani ambao hawakupigiwa upatu na kuzua mshangao mkubwa kwenye ulimwengu wa masumbwi.

Tyson alitandikwa na James ‘Buster’ Douglas mwaka 1990, na Lewis alichapwa na Hasim Rahman mwaka 2001.

Na haikuwa bahati mbaya kwa Joshua kwani alikuwa amepigwa kutoka raundi za kwanza alipomuangusha Ruiz.

Na baada ya kupigwa ngumi kali ya kushoto, Joshua aliangukia kamba za ukumbi wa ndondi .

Na kabla ya kukamilika kwa dakika tatu za raundi hiyo aliangushwa tena bada ya Ruiz kumshambulia kwa mchanganyiko wa makonde.

Hatua hiyo iliwashangaza wengi katika ukumbi wa Madison Square Garden.

STREET QUIZ:DIAMONDPLATNUMZ NI RAIA WA NCHI GANI KWA SASA BAADA YA KUWA MAARUFU? MWANZA

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

1 Comment

  1. Pingback: Andy Ruiz Junior Atwaa Taji La Ubondia Wa Dunia Baada Ya Kumtwangwa Anthony Joshua! – News Blog

Leave a Reply