MICHEZO

Sasa Baasi Chelsea Wamekubali Kumuachia Mshambuliaji Gonzalo Higuan!

on

Baada ya kuondolewa kwa Alvaro Morata na kuletwa mshambuliaji Gonzalo Higuan kutoka AC Milan alipokuwa akicheza kwa mkopo akitokea Juventus, wengi walijua tu kocha wa Chelsea Maurizio Sarri anafanya hviyo kwa ajili ya kumtengenezea mazingira Higuan ya kuja kupata nafasi.

Higuan ambaye alikuwa anatajwa kama kipenzi cha kocha Maurizio Sarri waliyewahi kufanya nae kazi Napoli ameshindwa kuonesha kiwango bora toka amewasili Chelsea kwa mkopo na sasa wanataka kumrudisha katika club yake ya Juventus baada ya kukiri kuwa hawaoni kama wanaweza wakarefusha mkopo wake.

Gonzalo Higuan toka amewasili Chelsea kwa mkopo wa miezi sita January 2019 amecheza game 21 na kufunga magoli 5 pekee, makubaliano ya awali yalikuwa na kipengele cha kurefusha mkataba wake wa mkopo kwa pound milioni 15.7 au Chelsea kumnunua jumla kwa pound milioni 31.6

HIGHLITS Mji Mpwawa 2 -1 Mkurugenzi fc

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you