HABARI ZA MASTAR

Ben Breaker: Hakuna Star Yeyote Wa Kike Tanzania Anayenivutia Kimapenzi 

on

Wakati wanamitindo wengi wa kiume Tanzania wakijipatia majina makubwa na umaarufu kutokana na kutoka kimapenzi na Wasichana maarufu Tanzania wakiwemo waigizaji wa Filamu Tanzania(Bongo movies)

Lakini hii imekaa tofauti kwa Mwanamitindo Ben Breaker ambae yeye kajizolea umaarufu kutokana na kazi zake zenye ubunifu na kushinda tuzo za kimataifa Mwanamitindo huyo ameeleza kuwa hakuna star wa kike Tanzania anayemvutia kimapenzi kutokana na mastar hao kutokuwa na uhalisia ukiwaona kwenye mitandao yao tofauti na jinsi walivyo katika maisha halisi

Ben Breaker ameeleza kuwa wengine kwenye mitandao huonekana wazuri na wenye mvuto ila ukikutana nao katika maisha halisi wanapoteza mvuto na uzuri uonekanao kwenye mitandao hivyo hawamvutii kabisa.
“kutoka nao kimapenzi ni bora atoke kimapenzi na Wasichana wasio na umaarufu kuliko kuwa na mahusiano na wasichana maarufu Kutoka Tanzania”.Alisema Ben Breaker.

STREET QUIZ IN ST. JOHN UNIVERSITY DODODMA SEASON TWO

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you