HABARI ZA MASTAR

Chris Brown Aweiweka Rekodi Kwenye Muziki wa RnB

on

Inaelezwa kuwa Mwimbaji wa miondoko ya RnB Chris Brown anazidi kuweka rekodi kubwa kwenye industry nzima ya muziki wa R&B kwa ujumla ikiwa leo ametangazwa  kufikisha jumla ya mauzo ya album milioni 91.5 kwa Marekani pia nakala milioni 130 duniani kote.

Hii inamfanya Chris Brown kuwa moja ya wasanii wa R&B ambao wanashikilia namba 1 ya mauzo kwa muda wote. Siku kadhaa zilizopita iliripotiwa kuwa mkali huyo aliweka rekodi nyingine ya kufikisha wiki 400 ndani ya chart za album (Billboard 200) baada ya album yake iliyopita ‘Heartbreak On A Fool Moon’ kufikisha wiki ya 77 mpaka sasa tangu itoke October 31, 2017 ikiwa na jumla ya ngoma 45.

Na Inaelezwa pia Chris Brown yupo mbioni kuachia Album yake ya tisa inayofahamika kama ‘Indigo’ ambayo inatajwa kuachiwa rasmi June 21,2019 ikiwa na jumla ya ngoma 30, Album hiyo inatajwa kujumuisha ngoma ambazo tayari zimeshaachiwa ikiwemo“Undecided,” “Back to Love”

HIGHLITS Pan Africa 2 – 2 Mbuni fc full Goals

TOA MAONI YAKO HAPA

Leave a Reply