KITAIFA

Endapo Serikali Itashindwa Kuleta Maji Jimboni Kwake,Mbunge Atishia Kuleta Vurugu

on

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji jana Mei 2, bungeni jijini Dodoma, Kadutu amesema jimbo lake kwa muda mrefu limetengwa na halipewi kipaumbele huku wananchi wake wakitaabika kwa ukosefu wa maji.

Mheshimiwa Waziri na wataalam mlioko hapa nyuma yangu hebu fanyeni mnavyoweza, je tutatengwa hadi lini?, sisi sio wakimbizi kama hamtaki kutupa tawala za mikoa tupeni maji, wataalam msikie tutaleta vagi hata wao hawatakanyaga huko,” amesema Kadutu.

Akizungumza kwa hisia kali, Kadutu amesema yeye na wananchi wanakwenda kuziba Mto Malagalasi kwa sababu mradi wa Mto huo badala ya kuhudumia pia wananchi wa Ulyankulu, umeelekezwa Kaliua na Urambo mkoani Tabora.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you