KIMATAIFA

Bob Wine Aachiwa Kwa Masharti Magumu Kesi Yake Yaendeshwa Kwa Njia Ya Video Mwenyewe Akiwa Gerezani,Awasiliana Na Hakimu Kupitia Teknolojia Hiyo

on

Msanii na mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi ameachiwa kwa dhamana na mahakama mjini Kampala japo kwa masharti makali.

Mchakato wa kulisikiliza ombi lake la dhamana uliendeshwa kwa njia ya video akiwa gerezani Luzira. Aliweza kuwasiliana na hakimu kupitia mawasiliano hayo ya video, hatua ilioepusha kutokea kwa vurugu kama ilivyotarajiwa iwapo angasafirishwa hadi mahakamani.

Ameshtakiwa kwa kushiriki katika maandamano ya ‘haramu’ mnamo mwaka jana ya kupinga kodi ya kutumia mitandao ya kijamii maarufu Uganda kama OTT.

Wafuasi wa mbunge Robert Kyagulanyi walionekana wakiimba wimbo wao wa ushindi baada ya hakimu wa mahakama ya Buganda Road kukubali ombi la Bobi Wine kupewa dhamana.

Uamuzi huo ulitolewa katika kikao kilichochukua muda wa saa nne, upande wa serikali ukipinga apewe dhamana.Kabla ya hakimu kumpatia dhamana, Bobi Wine alipewa fursu ya kuzungumuza:

‘Napenda kusisitiza kwamba sio mimi ninayeshitakiwa mahakamani ni mahakama yenyewe, maamuzi ya mahakama itakayotowa sio tatizo kwangu, mimi nitaendelea na kusema ukweli.

‘Kazi yangu ni kutetea haki, kazi yangu ni kupigania haki yako wewe hakimu na mimi na raia wengine wa Uganda. Kama itakuwa haki mimi kubaki hapa korokoroni, nitamushukuru mwenyezi Mungu kwa sababu nina kazi nyingi za kufanya hata hapa gerezani’ alisema mwansiasa huyo wa upinzani.

Masharti magumu aliopewa Bobi Wine:

Kyagulanyi amepewa masharti magumu ya dhamana kulingana na umarufu wake anapopita mjini anakuwa na wafasi wakubwa wakimufatilia, na katika masahriti hayo amekatazwa kuhusika katika mkusanyiko au Maandamano kama anavyosema wakiri wake Asumani Basalilwa:

‘Haya masharti yanashangaza kwasababu ni nani ana uwezo wa kusema maandamano ni mazuri au mabaya?

‘Kama hiyo nguvu wanajipatia polisi rafiki yetu Bobi wine asiwe huru nchini mwetu, Kwasababu polisi wanaweza kukamata watu bila mpango, wanaweza kukukamata ukiwa unafanya kazi yako unaenda kula, wanakukamata. Kama ni mahakama itasema mkutano huu ni haramu, hivyo ni vizuri lakini kama ni polisi, kutakuwa na vita vingi,’ amesema Asuman.

Licha ya mashariti aliyopewa, Mawakili wake hawakufurahishwa na mfumo wa mahakama uliotumiwa wa teknolojia bila ya kuwasiliana na mteja wao akiwa Luzira:

‘Sio teknolojia mbaya, lakini leo sheria yetu Uganda inasema, ni lazima uje mahakama uwasilishe ombi kama unataka kufanyisha video conference. Lakini hakuna aliyekuja hapa kuwasilisha ombi hilo, kwa hivyo kilichofanyika hapa ni kinyume cha sheria’.

Watu waliokuwa mahakamni hawajafurayishwa na maamuzi ya mahakama jinsi serikali inavyomunyima haki za kufanya kazi Robert Kyagulanyi.

‘Hakuna demokrasia hapa, kila anayetaka kuwa rais anawekwa mahabusu’ ameeleza raia mmoja aliokuwepo nje ya mahakama Kampala.

Kampeni mpya ilianzishwa katika mitandao ya kutaka Bobi Wine aachiliwe huru huku baadhi wakizungumzia hatua hiyo kama ya kutia wasiwasi.

Mashirika ya kutetea haki za binaadamu likiwemo la Marekani, Tom Lantos Human Rights Commission, na shirika linaloshinikiza uongozi wenye maadili na demokrasia kwa wote – Vanguard Africa, yameshutumu hatua hiyo ya serikali ya Uganda.

Bobi Wine alikamatwa siku ya Jumatatu wakati akilipokuwa njiani kupeleka barua makao makuu ya polisi kuwafahamisha anakwenda kufanya mandamano ya kumunyima haki zake za kufanya kazi yake ya muziki ikiwa tangu mwaka jana wamezuia matamasha 124.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply