HABARI ZA MASTAR

Birthday Ya Ruge: “Nandy Alimpenda Sana Baba”Mwachi Afunguka

on

Leo Mei Mosi ambayo ni siku ya wafanyakazi ni siku ya kuzaliwa ya marehemu Ruge Mutahaba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media. Alifariki dunia Februari, 26 akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini na baada ya siku chache kuzikwa nyumbani kwao Bukoba.

Leo ni siku yake ya kuzaliwa ambapo wadau mbalimbali wakitoa salamu zao ambapo shughuli ya ibada itafanyika nyumbani kwao Bukoba.

Katika maandalizi ya shughuli hiyo, Mwachi ambaye ni mtoto wa marehemu amefunguka kwa mara ya kwanza kumzungumzia muimbaji Nandy ambaye ameonekana kuwa karibu zaidi na familia hiyo.

“Nandy alikuwa ana uhusiano na baba yangu,” alisema Mwachi . “Nimeanza kumjua kupitia hilo ingawa alikuwa msanii wa THT, kwahiyo kwa familia tumemfamu kama mpenzi wa baba wangu na alikuwa ana muheshimu sana baba yangu na sisi tumeamua kumheshimu,”

Hata hivyo Caby ambaye ni mmoja kati ya binti ambaye alizaa mtoto mmoja na marehemu ameandika ujumbe mrefu kuhusiana na baba watoto wake huyo.

“Happy Birthday Babe… Nothing Is the Same without You Love ❤️
😭😭😭😭😭😭😭 #Ruge #BabaTravis @travis_mutahaba #LoveofmyLife #RestinPeaceBabe #Tutaonana
Nimezoea every of your birthday lazima uje home.. and unichukue and twende sehemu then turudi home tulale.. bt now it’s not the same anymore Ruge… 😭😭😭😭😭 And Am sitting here crying by my self.. I miss you.. God will tell you that.. I swear upon him.. I Miss You Babe 😭
Umeniacha na Travis Wangu.. 😭😭😭😭 nimlee mwenyewe 😭😭😭😭 Baba Travis 😭😭😭,”

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you