ELIMU

Utamaduni Wa Sokwe Unapotea Kwasababu Ya Binaadamu,Mambo 6 Ya Usiyo Yajua Kuusu Sokwe

on

Huenda tunafikiria kwamba utamaduni ni wa binaadamu pekee lakini wanyma apia wanaweza kuwna autamaduni wao.

Licha ya kwamba tabia nyingi hutokana na jeni, baadi ya viumbe wanaweza kujifunza mambo mapya na uyapasisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Sokwe katika maeneo mengi wametambua mbinu ngumu na nzito za kutumia vyenzo kutafuta chakula, maji na kuwasiliana – na mbinu hizi kufunzwa watoto wao kijamii.

 

Lakini utafiti mpya umedhihirisha kwamba elimu hii inatishiwa kutokana na shinikizo katika maazi ya wanyama hawa unaotokana na – wewe – binaadamu.

Watafiti katika taasisi ya utafiti wa wanyama Evolutionary Anthropology, nchini Ujerumani na utafti kuhusu uhai anuai (iDiv), umegundua kupungua kwa 88% kwa tabia za jamii za sokwe ulioathirika pakubwa kutokana na binaadamu barani Afrika, ikilinganishwa na maeneo yalio na idadi ndogo ya binaadamu.

Hizi ni tabia sita za sokwe zinazopungua kutokana na athari ya binaadamu:

 1. Kuvuwa Mwani baharini kwa gongo

Mara nyingi sokwe hutumia vyenzo kutafuta au kula chakula, lakini kuna utofuati wa vyombo wanavyochagua kwa matumizi yapi katika maeneo wanayoishi

Mnamo 2014 na 2015, Watafiti katika chuo cha Max Planck Institute wamegundua sokwe hutumia vyenzo virefu na madhubuti kuvua mwani huko Bakoun, Guinea.

Kwa mujibu wa Dkt Kalan, sokwe kutoka eneo la karibu huko Bossou, Guinea, pia huvuwa mwani kwa kutumia vjiti virefu vya takriban mita nne

Tabia hiyo ilikuwa tofuati na ripoti za awali za uvuvi wamwani nchini Congo.

 1. Kufunza namna ya kutafuta mchwa

Mnamo 2016, kundi la wanasayansi wa kimataifa walikusanya ushahidi wa kwanza wa sokwe wa msituni wakiwa funza watoto wao namna ya kutafuta mchwa kwa kutumia kijiti. Sio jambo la kawaida kuwaona wanyama wakifunza kitu.

Sokwe katika mbuga ya kitaifa ya Nouabalé-Ndoki katika Jamhuri ya Congo, walitengeneza vijiti hivyo kutoka aina fulani ya mimea na waliziunda kwa umbo lenye brashi kwa juu.

Katika mifano ilionaswa kwenye kamera, mama sokwe kwa mara nyingine walileta vijiti hivyo kwa wingi katika tundu la mchwaa na mara nyingine kuwapa watoto wao nusu ya kijiti na nusu nyingine wakakishikilia wao na kuwafunza watoto wao namna ya kujitafutia chakula.

 1. Kurusha mawe

Baada y kugundua mkusanyiko wa mawe karibu na mti katika maeoe manne ya utafiti huko Afrika magharibi, watafiti wa waliweka mitego ya kamera na wakagundua tabia ambayo haikujulikana awali ya sokwe, mbinu ya kukusanya mawe chini ya miti.

Wanasayansi walishangazwa kuona wanyama pori huko Boé, kusini mashriki mwa Guinea-Bissau, wakiyarushia miti mawe na kurudi mara kwa mara kuyatembelea maeneo hayo.

Tabia hii imedhihirika Afrika magharibi pekee.

 1. Kuvunja kokwa

Mnamo 2012, watafiti katika taasisi ya Max Planck waligundua namna makundi matatu ya sokwe huko Ivory Coast walitumia mawe kuvunja kokwa za njugu.

Msimu wa njugu ulipoendelea, ziliishia kuwa kavu na rahisi kuzivunja, makundi mawili yagaukia kutumia vigongo ambavyo ni rahisi kuvipata msituni – lakini kundi la tatu likaendelea kutumia mawe.

Mtafiti Dkt Luncz amesema: ” Kwa binaadamu, utofauti wa kitamaduni ni sehemu muhimu katika kututofautisha makundi tofuati ya watu wanaoishi katika mazingira sawa.

“Hili linaonyesha kwamba sokwe wana uwezo sawa na sisi katika utofauti wa utamaduni.

 1. Kunywa maji kwenye mti

Sokwe hutengeneza vijiti vinavyowawezesha kukusanya maji kutoka tundu za mtini wakati wa msimu mkavu katika mbuga ya kitaifa ya Comoé nchini Ivory Coast.

Watafiti waligundua kwamara ya kwanza tabia hii mnamo 2014 na 2015.

ikilinganishwana mbinu nyingine walizutumia kukusanya asali, chungu na mchwa, vijiti hivyo vya kukusanya maji vilikuwa vinono na virefu zaidi, watafiti wanasema.

 1. Kuchimba ardhi kutafuta asali

Sokwe katika mbuga ya kitaifa ya Loango nchini Gabon, wanaweza kutumia vyenzo tofuati kukusanay asali kutoka kwenye mizingia ya nyuko na hutumia kati ya aina 3 na tano za vyenzo hivyo kukusanya chakula.

Wanasayansi walifurahishwa na namna sokwe hao waliweza kutafuta na kuchunguza mizinga ya chini ya ardhi ambayo sio rahisi kuyaona kutoka juu ardhini.

Kupungua kwa utofuati wa utamaduni

Wanasayansi wanasema utafiti zaidi unahitajika kubaini kwanini kila tabia inapungua lakini Dkt Kühl ameiambia BBC kwamba kupungu ahuko kwa jumla huenda kukweza kukafafanuliwa na mambo haya matano:

 1. Kupungua kwa idadi ya sokwe kunamaanisha jamii za sokwe zina uwezo mdogo wa kukumbuka jambo.
 2. Kugawanyika kijiografia kunatatiza mtiririko wa taarifa katika mazingira tofuati.
 3. Baadhi ya sokwe wanaonekana kuachana na tabia zinazowafanya kujulikana zaidi ili kuepuka kukumbana na binaadamu.
 4. Uhaba wa rasilmali unaotokana na maingiliano na binaadamu.
 5. Mabadiliko ya tabia nchi pia yanachangia uwepo wa rasilmali.

Dkt Kalan amesema: “Uchanguzi umebaini mfumo mzito na thabiti: sokwe wamepunguza utofuati wa tabia katika maenoe ambako kuna idadi kubwa ya binaadamu.”

“Mfumo huu uliokuwa endelevu, usiotegemea makundi ya aina za abia. Na kwa wastani utofuati wa tabia za sokwe ulipungua kwa 88% wakati kulikuwa na athari zinazotokana na binaadamu ikilinganishwa na maeneo ambao hakuna binaadamu wanafika.”

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you