KIMATAIFA

HIVI PUNDE:’Hali Ni Mbaya Kuliko Ilivyodhaniwa’ Nchini Msumbiji! (+VIDEO)

on

Hali kaskazini mwa Msumbiji ni mbaya kuliko ilivyodhaniwa, msemaji wa Umoja wa mataifa ameeleza, siku chache baada ya kimbunga Kenneth kutuwa nchini humo.

Kimbunga hicho kilituwa siku ya Alhamisi kwa upepo mkali wenye kasi ya 220km/h (140mph) kilichoviangamiza vijiji.

Takriban watu 700,000 sasa wanadhaniwa kuwa katika hatari katika eneo hilo wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha.

Pemba, mji mkubwa wa jimbo la Cabo Delgado kumeshuhudiwa mvua yenye kina cha mita mbili na mafuriko.

Msemaji katika ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinaadamu (Ocha) Saviano Abreu ameeleza kwamba hali ni mbaya katika miji ya Macomia na Quissanga, akiongeza kwamba kuna wasiwasi pia kwa kisiwa kisichoweza kufikiwa cha Ibo.

Mawimbi ya hadi mita 4 yanatarajiwa, na mashirika ya misaada yanahofia kwamba mvua itazidi kunyesha.

UTATA:Mwenyekiti Wa HALMASHAURI MBOZI VS Wenyeviti Wa Vitongoji Kuhusu Madai Ya Posho

MOZAMBIQUE FLOODS: Hali Bado Tete Nchini Msumbiji Wakumbwa Na Mafuriko

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you