KIMATAIFA

Familia Yamuozesha Binti Wa Miaka 10 Kwa Tsh Mil. 8, Ndoa Za Utotoni Bado Janga Duniani

on

Familia moja nchini Afghanistan imelazimika kumuozesha binti yao wa miaka 10 kwa dola $3,500 sawa na Tsh. Milioni 8 ili kusaidia matibabu ya kaka yake anayeugua maradhi ya kifafa.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, imeelezwa kuwa binti huyo aitwaye Nazanin alichumbiwa akiwa na miaka mitano iliyopita na alipofikisha mika 10 alikua mke wa mtu tayari.Mume wake ambaye ametoa mahari kwa sasa ana miaka 12.

Baba yake Nazanin hakutaka kupokea pesa hizo lakini hakua na budi” ameeleza mama yake Nazanin, ambaye anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Shahrake Sabz karibu na Mji wa Herat magharibi mwa Afghanistan.

Mama Nazinin amesema kuwa familia yake ina watoto saba, wasichana watatu na wavulana wanne, Na hakuna mtoto aliyefanikiwa kwenda shule na hali yao kiuchumi ni mbaya kwani hawana hata kazi.

Akielezea sababu za kumuozesha binti yao akiwa mdogo Mama huyo amesema “Kijana wetu wa kiume amekua akiugua maradhi ya kifafa tangu alipofikisha miaka minne na hatukua na hela za kugharamia matibabu yake, Kwa hiyo nilikubali kumuozesha binti yangu Nazanin na kutumia pesa za mahari nilizopata kumtibukaka yake.” .

Hata hivyo, mama huyo anajutia kwani mtoto wao hakufanikiwa kupona ugonjwa huo licha ya kutumia pesa nyingi kwenye matibabu.

Kwa upande wa baba wa mtoto huyo, amesema kuwa anajutia kwa kumuozesha mwanaye angali mtoto kwani amemnyima haki za msingi.

Mtu anapomuuza binti yake mdogo bila shaka atakuja kujutia hatua hiyo baadae. Mimi pia najuta, lakini nitafanya nini, kwani tayari imeshatokea.” ameeleza baba wa binti huyo.

Nchini Afghanistan, umri wa kisheria kwa wasichana kuolewa ni miaka 16, na wavulana ni miaka 18. Lakini wengi wanaozwa au kuolewa wakiwa chini ya miaka hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF ya mwaka 2018, Asilimia 35% ya wasichana nchini Afghanistan huolewa kabla ya wkufikisha miaka 18, na 9% huolewa kabla ya kufikisha miaka 15.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you