KITAIFA

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI:WANAFUNZI 133 SHULE YA SEKONDARI BUKIMA WALIOKOSA VYUMBA VYA MADARASA WAANZA MASOMO.

on

Wanafunzi wa shule ya sekondari bukima iliyopo musoma vijijini waliokuwa wamekosa nafasi ya kujiunga  na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa wanafunzi 133 wameanza masomo  hii ni baada ya kukamilika kwa vyumba viwili vya madarasa shuleni hapo.

Akizungumza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Elbert Deogratias amesema wanafunzi 187 walifaulu kujiunga kidato cha kwanza 2019 lakini waliopangiwa shule hapo ni wanafunzi 50 na kupelekea jumla ya wanafunzi 133 kukosa nafasi kwa sababu ya uhaba wa vyumba vya madarasa,

“Kukamilika kwa vyumba viwili vya madarasa shuleni hapa kumeruhusu wanafunzi waliokuwa nyumbani kuanza masomo yao mpaka sasa tuna madarasa matatu na kila darasa wanakaa wanafunzi 62 “alisema Elbert.

Diwani wa kata ya Bukima January Simula amewataka wadau kushirikiana katika sekta ya elimu na maendeleo kuhakikisha wanaondoa tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa, huku  akimshukuru Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kutoa kipaumbele kwa shule za sekondari ili kukamilisha madarasa na kila mwanafunzi aliyefaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo,

Ambapo tumepokea jumla ya mifuko ya saruji 150 ambayo 50 kutoka ofisi ya Mbunge, mabati 54 na saruji 100 kutoka mfuko wa jimbo kwaajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa.

Aidha ujenzi wa vyumba vya madarasa na sekondari ya Bukima umeshirikisha nguvu za Mbunge wa Musoma vijijini na ushirikiano wawananchi wa vijiji vya Bukima,Kastam na Butata.

UTATA:Mwenyekiti Wa HALMASHAURI MBOZI VS Wenyeviti Wa Vitongoji Kuhusu Madai Ya Posho

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you