KIMATAIFA

Chanzo Cha Moto Kanisa Kuu La Notre Dame Kuungua Moto Mjini Paris Chaelezwa

on

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wamesema leo moto ulioteketeza kanisa kuu mjini Paris la Notre Dame ulikuwa ajali ya kawaida.

Wakati Ufaransa inahuzunika kufuatia kuharibiwa kwa moja ya alama zake muhimu. Mkuu wa Idara ya Mashtaka mjini Paris Remy Heitz amesema hakuna ishara yoyote kuwa tukio hilo la moto uliozuka jana jioni katika kanisa la Notre Dome lilikuwa la kupangwa.

Kwa mujibu wa DW. Rais wa Ufaransa Emanuel Macron ameahidi kulijenga upya kanisa hiyo ambalo linazingatiwa kuwa kivutio muhimu barani Ulaya. Salamu za pole zimeendelea kutolewa kutoka kote duniani ambapo Papa Francis na Malkia wa Elizabeth wa Pili wa Uingereza wamekuwa viongozi wa karibuni kabisa kuelezea masikitiko yao kuhusiana na mkasa wa Notre Dame.

Wakati huo huo waziri wa utamudini wa Ufaransa amesema turathi muhimu zilizokuwemo ndani ya kanisa hilo zimeokolewa ikiwemo mabaki ya taji la miba linaloaminika kuwa alivyalishwa Yesu Kristo na sanamu la mtakatifu Louis.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply