MICHEZO

TETESI:Fahamu Fununu Za Soka Barani Ulaya Leo April 15, 2018, Zidane, Dembele, Alderweireld, Icardi, Werner, Zaniolo, Pepe

on

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa klabu hiyo huenda ikawauza wacheza muhimu mwisho wa msimu huu.

Raia huyo wa Ufaransa anataka kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake baada ya msururu wa matokeo mabaya msimu huu.. (Sky Sports)

Manchester United hawana hamu na mshambuliaji wa zamani wa Lyon Moussa Dembele.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amefunga magoli 18 katika mashindano yote msimu huu. (Mirror)

Arsenal wanataka kumsaini beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30. (Talksport)

Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi anatarajiwa kuondoka Inter Milan msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 huenda akahamia Real Madrid kwa dau la £52m. (AS)

Mchezaji anayelengwa na Liverpool na Bayern Munich Timo Werner hatotia saini kandarasi mpya na klabu ya RB Leipzig.

Kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 katika klabu hiyo ya Bundesliga inakamilika mwisho wa msimu huu. (Sky Germany)

Chelsea itashindana na Real Madrid katika mbio za kumnunua ,mshambuliaji wa Borussia Dortmund 19 na Sweden Alexander Isak. (Sun)

Hatahivyo Zidane mwenye umri wa miaka 46 amepinga madai kwamba atamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 31. (Marca)

Na timu hiyo itamuuza beki wa Ufaransa Raphael Varane, 25, kwa dau la £437m kutokana na sheria inayomzuia katika kandarasi yake . (RAI Sport via Calciomercato)

Bayern Munich wanamtaka kiungo wa kati wa Roma na Itali Nicolo Zaniolo mwenye umri wa miaka 19. (Bild – in German)

Rais wa klabu ya Lille Gerard Lopez anasema kuwa winga wa Ivory Coast ,23, Nicolas Pepe, ambaye ananyatiwa na Manchester United, ataondoka katika klabu hiyo ya Ufransa mwisho wa msimu huu . (Manchester Evening News)

Leicester imewachukua vijana watatu ili kusaidia kuendeleza timu hiyo katika siku za usoni.

Kiungo wa kati wa Guiseley Dylan Barkers, Beki wa Hasting United Jamie Fielding na kiungo wa kati wa Hasting Adam Lovatt wamejiunga na klabu hiyo. (Leicester Mercury)

Wawakilishi kutoka Manchester United, Juventus na Paris St-Germain walizuru klabu ya Aves ili kumtazama kiungo wa kati wa Sporting Lisbon ,24, Bruno Fernandes. (A Bola)

Kundi moja la wafanyibiashara linaloungwa mkono na European Money liko tayari kuinunua klabu ya Huddersfiedl Town kwa kitita cha £50m. (star)

ON TARGET 01 WITH SAM B DADY:NITAUA WOTE ATABAKI MTOTO WANGU TU!

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply