MICHEZO

Kumbe Mama Yake Lukaku Ni Shabiki Mkubwa Wa Messi Apagawa, Ashindwa Kuamini Baada Ya Kukutana Uso Kwa Uso Na Messi ‘”Oh Messi, Messi”

on

Inawezekana ukashindwa kuamini kama mama mzazi wa mchezaji maarufu duniani na anayecheza kwenye ligi kubwa kama ya Uingereza anaweza kuwa bumbuwazi na mshangao mkubwa kwa kukutana na nyota Lionel Messi.

Ila ni kweli hali hiyo imeweza kumkuta mama mzazi wa Romelu Lukaku ambaye alishindwa kuamini kile alichokiona machoni mwake, pale mchezaji bora kabisa duniani Lionel Messi alipokuwa mbele yake na kupata mshangao huku akiomba kupiga naye picha.

Kipande cha video kimeenea kwenye mitandao mbalimbali ambacho kikimuonyesha mama huyo, Adolphine Lukaku akiwa na mshangao huo mara baada ya kukutana na Messi wakati alipokuwa Old Trafford wiki iliyopita kwenye mchezo wa Champions League hatua ya robo fainali na timu yake ya Barcelona ikiibuka na ushindi wa baoa 1 – 0 dhidi ya wenyeji Manchester United.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply