KIMATAIFA

Awad Ibn Auf Kiongozi Wa Mapinduzi Ya Sudan Amejiuzulu

on

Mkuu wa baraza la Jeshi la Sudani amejiuzulu siku moja baaba ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir yaliyosababishwa na wimbi la maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.

Waziri wa ulinz Awad Ibn Auf alitangaza uamuzi huo kwenye TV, na kumtaja mrithi wake Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan.

jeshi limesema kuwa litaendelea kuwa madarakani kw amiaka miwili na baadae utafanyika uchaguzi.

Lakini viongozi wa maandamano wanasema hawataondoka mitaani hadi jeshi litakapokabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia.

Kuanguka kwa Bwana Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza mwezi Disemba mwaka jana ambapo waandamanaji walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu.

Bwana Ibn Auf alikuw amkuu wa ujasusi katika jeshi wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007.

Kiongozi wa kijeshi ambaye amechukua mamlaka kwa sasa anacheo cha juu pia kijeshi, lakini kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press rekodi yake ni safi kuliko majenerali wengine wa Sudan .Amesemekana pia kukutana na waandamanaji kusikiliza maoni yao.

Bwana Bashir anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu juu ya mzozo wa Darfur.

hata hivyo baraza la jeshi limekwoishasema kuwa halitampeleka bwana bashir kwenye mahakama hiyo, ambaye anakana mashtaka yote dhidi yake , ingawa anaweza kushtakiwa katika mahakama za Sudan.

Jinsi sakata la hivi karibuni lilivypotokea

Licha ya kung’olewa mamlakani kwa Bwana Bashir siku ya Alhamisi, waandamanaji wamegoma kuondoka mitaani, huku wakiendelea kukita kambi kweny makao makuu ya jeshi mjini Khartoum, wakikaidi amri ya kutoitoka nje iliyowekwa na jeshi.

wameendelea kuwepo kwenye mitaa ya Khartoum usiku kucha

Katika hatua yao ya mwanzo kufuatia maandamano hayo, baraza la kijeshi lilijitokeza na kukanusha kwamba halitaki mamlaka , likiwaambia waandamnaji kuwa wataamua hali ya baadae ya nchi yao, huku jeshi likiiimarisha usalama wa umma.

Saa chache baadae, bwana Ibn Auf akatangaza kuwa anajiuzulu na nafasi yake itachukuliwa na Luteni Jenerali Burhan.

“Ili kuhakikisha kunakuwepo na maelewano ya mfumo wa usalama, na hususani kwa majeshi na kwa kumtegemea Mungu ngoja tuanze njia ya mabadiliko ,” alisema.

Waandamanaji walisherehekea kuondoka kwake ghafla lakini Chama cha wasomi wa Sudan , ambacho kimekuwa kikiongoza maandmano, baadae kilitangaza kuwa mgomo wa kuketi mbele ya makao makuu ya jeshi utaendelea.

“Tunaowatolea wito wanajeshi wote kuhakikisha kwamba wanakabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia ,” walisema kwenye ukurasa wao wa Facebook.

Aidha walitoa wito wa kuondolewa kwa “maamuzi dhalimu ya viongozi ambao hawawakilishi watu ” na kuondolewa kwa “nembo zote za utawala ulioondolewa mamlakani ambao ulihusika katika uhalifu dhidi ya watu”.

“Hadi madai haya yatakapotimizwa tuhtaendelea na maandamano yetu ya kuketi chini kwenye makao makuu ya jeshi ,” ilisema ripoti ya chama hicho cha wasomi wa Sudan.

Wakati huo huo polisi wamesema kuwa watu wapatao 16 waliuawa kwa risasi katika maandamano ya Alhamisi na Ijumaa.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you