MICHEZO

Tetesi Za Usajiri Wa Soka Ulaya Jumanne 09.04.19: Rice, Pogba, Adams, Clyne, Acosta, Carroll

on

Manchester United kutangaza dau la usajili la pauni milioni 50 ili kumnasa kiungo kinda wa West Ham Declan Rice,20. (Irish Independent)

Rice, amesema kujiunga na West Ham ulikuwa uamuzi bora kabisa aliowahi kuufanya baada ya Chelsea kumtema akiwa na miaka 14. (Standard)

Beki wa kushoto wa Ajax Nicolas Tagliafico, 26, amesema kuwa mwisho wa msimu huu utakuwa ni muda muafaka wa kuhamia kwenye Ligi ya Premia. Beki huyo raia wa Argentina anawindwa na Arsenal. (Mirror)

Kocha msaidizi wa Manchester United Mike Phelan amesema kiungo wa klabu hiyo Paul Pogba, 26, “bado hajamaliza kazi yake” na anamtaka mchezaji huyo kusalia Old Trafford. (Telegraph)

Pogba anaendeleakugonga vichwa vya habari akihusianishwa na uhamisho kwenda Real Madrid mwishoni mwa msimu.

Jarida la ‘France Football’ la nchini Ufaransa klinamshawishi Pogba kuhama Old Trafford na kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu. (France Football – in French)

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema klabu yake ilitaka kumsajili Pogba kutokea Juventus lakini ilishindwa kufikia dau la United mwaka 2016. (ESPN)

Everton wanajiandaa kutangaza dau la usajili ili kumnasa mshambuliaji wa Birmingham City Che Adams, 22. (Football Insider)

West Ham hawatampatia Andy Carroll, 30, mkataba mpya mwishoni mwa msimu. Mshambuliaji huyo amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu, hali inayomfanya kushindwa kurejea dimbani mpaka msimu utakapokwisha. (Mail)

Wagonga nyundo hao wa London watapambana na Bournemouth ili kumsajili beki wa Liverpool Nathaniel Clyne, 28. Clyne yupo kwa mkopo Bournemouthtoka mwezi Januari. (Goal)

Kiungo wa DC United na Argentina Luciano Acosta, 24, amesema kuwa ana furaha kunyemelewa na Manchester United.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply