MICHEZO

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Madrid Waandaa Dau Nono Kwa Pogba,United Kumenoga Ole Gunnar Solskjaer Afichua Siri Za Mawakala

on

Real Madrid wanapanga kutoa kitita cha pauni milioni 125 ili kumsajili kiungo Paul Pogba mwenyeumri wa miaka 26, kutoka Manchester United. (Sun)

Chelsea wanapanga kumpatia Callum Hudson-Odoi kandarasi mpya ya mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki ili kumshawishi mchezaji huyo kinda mwenye miaka 18 asiondoke klabuni hapo. (London Evening Standard)

Klabu ya Wolves wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa streka Raul Jimenez, 27, kutoka Mexico kwa rekodi ya usajili ya klabu hiyo ya pauni milioni 25. (Telegraph)

Kocha Carlo Ancelotti amesema Napoli hawatalazimika kumuuza beki wao mwenye thamani ya pauni milioni 130 Kalidou Kouliably, 27, ambaye amekuwa akiwindwa na Manchester United kwa muda mrefu. (Mail)

Ole Gunnar Solskjaer amefichua siri kuwa mawakala wengi wamekuwa wakiwasiliana na Manchester United ili kujaribu kuhamishia wachezaji wao kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Sky Sports)

Ila wachezaji Jadon Sancho, 19, wa Borussia Dortmund na beki wa Real Madrid’s Rafael Varane, 25, ndiyo wanaopigiwa upatu zaidi kujiunga na Manchester United katika msimu ujao wa usajili. (Independent)

Miamba ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich wanapanga kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kuwekeza pesa nyingi zaidi katika dirisha la usajili la mwisho wa msimu huu. (Marca)

Arsenal wanaripotiwa kufanya mazungumzo na Barcelona ili kumsajili beki wao Samuel Umtiti, 25. (Gazetta dello Sport, via Mirror)

Kocha mpya wa Leicester City Brendan Rodgers amesema klabu hiyo itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa wachezaji wao nyota watasalia klabuni hapo mwishoni mwa msimu. (Leicester Mercury)

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply