HABARI ZA MASTAR

Ommy Dimpoz Aeleza Alivyokuwa Anajisikia Alivyoona Mitandaoni Wameandika Ommy Dimpoz Amefarika

on

Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva Omary Nyembo alimaarufu Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu muziki wake na kusema kuwa ana kolabo nyingi sana.

Akiongea katika kipindi cha Clouds360 cha Clouds Tv, msanii huyo amesema kuwa katika nyimbo zake ambazo tayari amezifanyia video ziko 12 na katika nyimbo hizo ameachia nyimbo mbili tu.

Mbali na kuiongea hicho pia alisema ‘”Sikuwaza kuimba niliwaza maisha yangu ya kawaida nitaishi vipi” Nilivyokuwa naumwa na sauti haitoki iliniumiza katika maisha ya kawaida nitaishi vipi maana kama nipo chumbani na mtu yupo jikoni nitamuitaje anisikie na ukizingatia sauti ilikuwa ndogo na niliwaza ikija kupotea itakuaje, Sikuwaza kuimba kwa wakati ule ila niliwaza nitaishi vipi kwenye maisha haya ya kawaida”

“Sikuogopa kusingiziwa kufa bali niliwazia familia yangu “Wakati naumwa vile nilivyokuwa naona watu kwenye mitandao wameandika ‘OmmyDimpoz afariki dunia’ sikuwa nashtuka ila nilikuwa nawaza familia yangu ipo kwenye hali gani Mama yangu, Mama zangu wadongo, mashangazi na wengine maana mimi nipo nje ya nchi kwa matibabu wao wapo hapa na wao wanasikia na kukutana na maneno hayo sijui walikuwa wanayapokeaje, TCRA inabidi ifanye jambo kwa hawa watu wenye tv za online maana wengi wao huandika vitu ambavyo sio vya ukweli”

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you