HABARI ZA MASTAR

Cardi B Afunguka Jinsi Alivyokuwa Akitumia Madawa, Kuwalewesha Wanaume Pindi Walipotaka Kushiriki Tendo La Ngono

on

Cardi B alijitetea baada ya picha ya video iliyokua ikizunguka akionekana akisema kuwa aliwalewesha na kuwaibia wanaume waliokuwa wakitaka kushiriki ngono naye wakati alipokua akifanya kazi ya kunengua kabla ya kuwa maarufu.

Mwanamuziki huyo wa miondoko ya rap alikosolewa baada ya video hiyo ya Instagram iliyorekodiwa miaka mitatu iliyopita kusambaa tena mitandaoni.

”Sijawahi kusema kuwa mimi ni msafi sana au natoka ulimwengu ulio mzuri sana”.Alisema mwanadada huyo.

Awali video hiyo ilirekodiwa wakati ndio ameanza kazi yake na lilikua jibu kwa mtu aliyesema kuwa hana haki ya kuwa mwenye mafanikio kwa kuwa hafanyi kazi yoyote.

”Hakuna nilichokua napata.Hakuna,” alisema kwenye video hiyo, kabla ya kuweka wazi kuwa alikua akiwaalika wanaume kwenye hoteli kabla ya kuwanywesha na kuwaibia.

Akijibu shutuma hizo , aliandika kwenye ukurasa wa Instagram alieleza kuwa alikua akizungumza mambo ambayo yalikwishapita mazuri au mabaya ambayo yalinisaidia kuishi”.

Aliongeza:”Mimi ni sehemu ya utamaduni wa hiphop ambapo unaweza kueleza wapi umetoka , na hata mambo mabaya uuliyoyafanya kufika ulipo leo.” Mshindi wa tuzo za Grammy pia alieleza kuwa kuna wanamuziki ambao wanasifu mauaji, vurumai, dawa za kulevya na wizi”.

Aliandika: ”Sikuwahi kujisifu kwa vitu vilivyojitokeza kwenye video, sikuviweka kwenye muziki kwa sababu sijivunii na ninawajibika kutosifia.

Cardi B alimaliza kwa kueleza wanaume aliowazungumzia kwenye video yake ya zamani kuwa walikua wanaume aliokua na mahusiano nao na walikua wanajua wanachokifanya”.

Mapema juma hili, Hashtag ya #SurvivingCardiB ilikua imesambaa -ikifananishwa na Makala ya R Kelly, iliyoeleza miaka ya shutuma za ngono dhidi yake.

Baadhi ya watuamiaji wa mitandao ya kijamii wanamfananisha na mchekeshaji Bill Cosby, ambaye alihukumiwa kifungo mwaka 2018 baada ya kushutumiwa kuwalewesha wanawake kwa madawa na kuwadhalilisha.

Wengine wa mitandao ya kijamii walimtetea Cardi B kwa kuwa muwazi.

Mapema mwaka huu,Cardi B aliweka historia alipokua mwanamke wa kwanza akiwa muimbaji wa peke yake kupata tuzo ya Grammy kwa kuwa na albamu bora ya muziki wa kufokafoka yenye wimbo wake wa Invasion of Privacy.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you