USAJIRI

Tetesi Za Usajili Barani Ulaya Jumatano Hii, Rashford, Mkhitaryan, Ozil, Sterling, Hazard, Rakitic na Wengine Sokoni

on

Barcelona wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza na Manchester United Marcus Rashford, 21. Mkataba wa mshambuliaji huyo na United utaisha 2020. (Mundo Deportivo – in Spanish). Barca wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 100 ili kumnasa Rashford. (Mirror)

Miamba hiyo ya La Liga inamouna Rashford kama mbadala wa muda mrefu kwa mshambuliaji wao nyota Luis Suarez, lakini United hawatazamiwi kumuuza mshambuliaji huyo. (ESPN)

Manchester United wanamnyemelea beki kinda wa klabu ya St-Etienne William Saliba, 18. (Le 10 Sport – in French)

Arsenal wana nia ya kuwauza viungo wake Henrikh Mkhitaryan, 30, na Mesut Ozil, 30, kama njia ya kupunguza gharama kubwa za mishahara za klabu hiyo. (Mirror)Real Madrid inapaswa kumsaini mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 24, badala ya kiungo wa Chelsea Eden Hazard, 28, anashauri kiungo wa zamani wa Blackburn Chris Sutton. (Mail)Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amesema kuwa “amechoshwa” na tetesi juu ya mustakabali wake. Mfaransa huyo mwenye miaka 28, amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa ikiwemo Barcelona na Manchester United. (Univision – in French)

Barcelona wanaweza wakamuuza kiungo Ivan Rakitic, 30, mwishoni mwa msimu huku Manchester United na Inter Milan wakitazamiwa kuwa watatupa karata zao ili kumnasa. (ESPN)

Liverpool wanajipanga kulipa ada ya usajili ya pauni milioni 10 ili kumnasa beki wa Norwich City Ben Godfrey, 21. (Football Insider)Kipa mkongwe raia wa Uhispania Iker Casillas, 37, ameongeza mwaka mmoja zaidi kwenye mkataba wake na klabu ya Porto na kusema atamaliza maisha yake ya soka na klabu hiyo ya Ureno. (Sky Sports)

Arsenal na Juventus ni miongoni mwa vilabu vilivyoonesha nia ya kumsaini beki wa kushoto wa Benfica Alejandro Grimaldo, 23, ambaye ni raia wa Uhispania. (Calcio Mercato)

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply