MICHEZO

Tetesi Za Usajiri Barani Ulaya Ijumaa Hii, Eriksen, Tierney, Pope, Mbappe, Fekir na wengine sokoni

on

Arsenal na Leicester zote zina hamu ya kumsajili mchezaji wa Celtic na mlinzi wa Scotland Kieran Tierney, mwenye umri wa miaka 21. Leicester inamtaka Tierney aichukue nafasi ya mlinzi Ben Chilwell wakati wakitarajia maombi kuwasilishwa kwa mchezaji huyo. (Mirror)

Gunners imefanya mazungumzo na winga wa zaidi ya miaka 21 wa Rennes Ismaila Sarr. Arsenal imeipiku klabu hiyo ya Ufaransa kufika katika robo fainali ya Ligi ya Uropa Alhamisi. (Goal France)

Burnley inatazamia kumuuza Nick Pope, wa miaka 26, kwa kiasi cha £10m msimu huu wa joto, huku Arsenal ikiwa na hamu kubwa ya kumsajili kipa huyo wa England. (Sun)Juventus itafanya kila iwezalo kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, mwenye miaka 20, kutoka Paris St-Germain msimu huu wa joto. (Tuttosport)

Newcastle ina hamu ya kumuajiri meneja wa Lyon Bruno Genesio iwapo Rafael Benitez hatoongeza mkataba wake huko St James’ Park. (L’Equipe)Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anataka kumsajili kiungo cha mbele wa Ufaransa na Lyon Nabil Fekir, mwenye umri wa miaka 25, katika msimu wa joto. (Daily Record)

Lakini Zidane hana hamu ya kumchukua mchezaji wa kiungo cha mbele wa PSG Neymar, wa miaka 27, kwenda Bernabeu. (AS)

Baada ya kumsajili mchezaji wa Brazil na Porto Eder Militao, Tayari Real imefikia kiwango cha mwisho kinachotakiwa cha wachezaji wasio raia wa Umoja wa Ulaya kwa mwaka ujao, na kufanya kuwa na uwezekano mkubwa kwa mchezaji wa Colombia, James Rodriguez kutojiunga nao punde tu mkataba wake wa miaka miwili utakapomalizika huko Bayern Munich. (Marca)

Real inataka kukusanya £128m katika mauzo ya wachezaji msimu huu wa joto na itaomba £42.7m kwa wachezaji Rodriguez na mchezaji wa kiungo cha kati wa Croatia Mateo Kovacic, kila mmoja, ambaye kwa sasa yuko Chelsea kwa mkopo. (El Confidencial)

Timu hiyo kuu ya Uhispania huenda ikatoa sehemu ya fedha hizo katika kumsajili mchezaji wa miaka 19 wa kiungo cha kati wa timu ya Roma Nicolo Zaniolo. (AS)Manchester United wamejiunga katika kutaka kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa PSG Adrien Rabiot, wa miaka 23. Raia huyo wa Ufaransa hana mkataba ifikapo msimu wa joto na tayari amezungumza na Barcelona, Arsenal, Chelsea na Tottenham. (Sun)

Aliyekuwa meneja wa Fulham Slavisa Jokanovic na bosi wa Preston Alex Neil ndio wanaopigiwa upatu kuijaza nafasi ya meneja wa timu ya West Brom. (Sky Sports)

PSG itamkabidhi meneja Thomas Tuchel mkataba wa mwaka mmoja zaida. Raia huyo wa Ujerumani alisaini mkataba wa miaka miwili mnamo Mei 2018.(L’Equipe)Aliyekuwa meneja wa Manchester United Jose Mourinho anasema hajahuzunishwa na kuteuliwa tena Zinedine Zidane huko Real Madrid. Mourinho, aliyehusishwa na kurudi katika timu hiyo kuu ya Uhispania amesema Zidane ndiye bora katika jukumu hilo. (El Chiringuito TV kupitia ESPN)

Meneja wa Huddersfield Jan Siewert amesema timu hiyo inayojikokota katika ligi kuu ya England huenda ikakabiliwa na mageuzi msimu huu wa joto. (Sky Sports)

Tottenham ilikaribia sana kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Ureno na kwa wakati huo mchezaji wa Porto Joao Moutinho mnamo 2012, anasema meneja Andre Villas-Boas. Moutinho, wa miaka 32, sasa anaichezea Wolves. (Talksport)Inter Miami ya aliyekuwa kapteni wa England David Beckham imetangaza inapanga kucheza huko Fort Lauderdale kwa misimu yake miwili ya kwanza. (NBC Sports)

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you