MICHEZO

Real Madrid Wamemtangaza Zinedine Zidane Kuwa Kocha Wao Kwa Mara Nyingine

on

Club ya Real Madrid ya Hispania leo imefikia maamuzi mazito ya kumrudisha tena aliyekuwa kocha wap Zinedine Zidane ambaye alijiuzulu kuendelea kuifundisha timu hiyo baada ya kudumu nayo kwa na kuipa mataji matatu mfululizo ya UEFA Champions League.

Zidane anarudi tena Real Madrid ambayo haina matumaini makubwa sana ya kutwa taji lolote kwa mkataba wa miaka mitatu, hiyo ikiwa ni miezi tisa toka atangaze kuondoka ndani ya club hiyo ya Real Madrid ambayo amepata nayo mafanikio akiwa mchezaji na kocha pia.

Real Madrid imemtangaza Zidane kuwa kocha wao wa tatu msimu huu baada ya kupoteza imani na Santiago Solari, mkataba huo sasa utamuweka Zidane ndani ya Real Madrid hadi 2022, tokeo 2015 Zidane akiwa na Real Madrid aliipa jumla ya mataji 9, matatu ya Champions League, Laliga 2016/2017, FIFA Club World Cup mara mbili na Super Copa Epana mara moja na UEFA Super Cup mara mbili.

DAVID KAFULILA APOKEA TAARIFA YA VIWANGO VYA RUSHWA MKOANI SONGWE

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *