HABARI ZA MASTAR

Msani Mkongwe Wa Bongo Fleva Dudu Baya Ashikiliwa Na Jeshi La Polisi!

on

Msanii na mlongwe wa muziki wa Bongo Fleva Godfrey Tumaini almaarufu Dudu baya anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay Jijini Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Mwananchi, Kamanda wa Polisi Kinondoni Mussa Taibu amesema Msanii huyo anashikiliwa kwa ajili ya mahojiano.

Ikumbukwe jana Waziri mwenye dhamana ya Habari Dkt. Harison Mwakyembe aliagiza Jeshi la Polisi lishirikiane na Basata kumchukulia hatua Dudu Baya kwa kosa la kumkashfu marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Ruge Mutahaba alipoteza maisha nchini Afrika ya Kusini kwa kudai kuwa alikuwa anawanyonya wasanii.

Baada ya amri hiyo Basata ilimtaka Dudu Baya kujisalimisha kituo cha Polisi Oysterbay asubuhi ya leo, na tayari ameshtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya mitandao.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply