HABARI ZA MASTAR

R Kelly Apata Dhamana Kupandishwa Mahakamani Machi 27.

on

baada ya kulipa dhamana ya $100,000, msemaji wa idara ya polisi ameeleza.Mapema Jumatatu alikana mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake wanne, watatu kati yao walikuwa ni watoto wakati wa uhalifu huo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 52 alionekana akiwa amevaa koti la samawati, hakuzungumza na waandishi habari aliposindikizwa kutoka gerezani na wakili wake.

Alijisalimisha kwa polisi Ijumaa na alisalia gerezani wikendi nzima.Muimbaji huyo amekabiliwa na tuhuma za unyanysaji kwa miongo kadhaa pasi kushtakiwa , na amekana tuhuma zote za awali.

Msemaji wa idara ya polisi Sophia Ansari amethibitisha Jumatatu kwamba R Kelly amelipa dhamana hiyo ya $100,000 ambayo ni 10% ya dhamana ya dola milioni moja iliyowekwa na jaji mwishoni mwa juma.

Kufika kwake mahakamani na kukana mashtaka hayo kunajiri wiki kadhaa baada ya makala ndefu kwa jina ‘Suriving R Kelly kupeperushwa. Ilituhumu unyanyasaji dhidi ya wanawake wengi, akiwemo aliyekuwa mkewe nyota huyo muimbaji.

Anashtakiwa kwa unyanyasaji unoadaiwa kufanyika tangu 1998.

Alikutana na mojawapo ya wanawake hao aliyekuwa anaadhimisha miaka 16 tangu kuzaliwa katika mgahawa mmoja – na mwingine ambaye pia alikuwa na umri wa miaka 16 – aliyeomba amtilie saini nakala ya kazi yake – au autograph.

Mahakama imemuagiza muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, asalimishe pasi yake ya usafiri na asiwasiliane na mtu yoyote aliye na umri wa chini ya miaka 18.

Inaarifiwa kwamba alipata tabu kulpa dhamana hiyo ya $100,000 iliyohitajika kutoka katika gereza la Cook County Jail.

Katika mkutano na waandishi habari baadaye, wakili maarufu Gloria Allred amesema kwamba sasa anawawakilisha wanawake sita wanaotuhumu kuwa muimbaji huyo aliwanyanyasa.

Aanatarajiwa kufika mahakamani Machi 27.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

10 Comments

 1. Dakota

  April 4, 2019 at 5:46 am

  It works very well for me

 2. Jonna

  April 17, 2019 at 3:54 am

  Thanks, it is quite informative

 3. Www.talkhelper.com

  April 17, 2019 at 9:06 am

  I like the article

  • Robert Ngonya

   April 17, 2019 at 9:14 am

   WELCOME!

 4. Norris

  April 17, 2019 at 2:51 pm

  I like the report

 5. This article

  April 18, 2019 at 9:37 am

  Thanks, it is quite informative

 6. Tisha

  April 18, 2019 at 9:02 pm

  I spent a lot of time to locate something such as this

 7. pocmicrosolutions.com

  April 24, 2019 at 9:13 am

  Thanks, it’s very informative

 8. Antonietta

  April 24, 2019 at 6:43 pm

  Thanks, it is quite informative

Leave a Reply