HABARI ZA MASTAR

Fid Q Awatolea Uvivu Walio Kimbia na Hela Za Rambirambi Ya Msiba Wa Godzilla

on

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amefunguka na kuwajia juu watu ambao wamekimbia na   Rambirambi ya msiba wa Godzilla.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Fid Q amesema kwamba wachangishaji walikuwa wengi, lakini baadhi ya michango ilifika ikiwemo iliyokusanywa na Niki Mbishi, Soggy Dogy na Wakazi, lakini wale waliochangisha kwenye vidaftari kuna baadhi hawakufikisha kabisa pesa hizo za rambi rambi.

Kwa taarifa nilizotoka nazo kule watu ambao wamefikisha ni washakaji zetu tu wale ambao walichangisha ka njia ya simu, kule twitter, ambao wamewasilisha ni kina wakazi na Niki mbishi, kulikuwa na wachangishaji wengi, kulikuwa wenye vidaftari, sasa wale wenye vidaftari kuna ambao walifikisha na kuna wengine hawajafikisha kabisaaa”.
Kutokana na hayo Fid Q amesema watu hao bado wana nafasi ya kuzirudisha na kuwasilisha kwa familia ya Godzilla, lakini wasipofanya hivyo Mungu ndiye atawahukumu.

Wito wangu kwa wote ni sawa tu kupita na rambi rambi, wajue ile ni rambi rambi watu wametoa kusaidia pale palipopungua, kwa hiyo bado muda wanao, watumie fursa hii kurudisha kisichokuwa chao, na kama hawatarudisha basi tumuchie aliyeumba wahukumu yeye“.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply