MICHEZO

Tetesi Za Usajari Balani Ulaya Leo Jumatano 20.2.2019

on

Manchester United wamemtaja winga wa klabu ya Borussia Dortmund Jaden Sancho, 18, kuwa mchezaji wanayemlenga zaidi, lakini wanahisi kwamba watalazimika kufuzu katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya msimu ujao ili kuweza kumnasa mchezaji huyo wa Uingereza. (Mirror)Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri atafutwa kazi iwapo klabu hiyo itashindwa katika fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili. (Mirror) Chelsea watamfuta kazi Sarri na kuweza kumlipa £5m – ikiwa ndio malipo ya kiwango cha chini zaidi kulipwa mkufunzi chini ya uongozi wa mmiliki Roman Abramovich. (Sun)

Chelsea imewalenga wakufunzi wa klabu ya Derby Frank Lampard na aliyekuwa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane kuwa warithi wa Sarri. (Sky Sports)Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anamchunguza kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 20, winga wa safu ya ulinzi upande wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21, na beki wa Leicester wa kushoto Ben Chilwell, 22, huku akiwa na mpango wa kuwanunua wachezaji wachanga wa Uingereza mwisho wa msimu huu. (Sun)

Timu ya Ujerumani Bayern Munich imejiunga na vilabu vingi vinavyomchunguza mchezaji wa Palace Wan-Bissaka. (Mail)

Manchester City wanatarajiwa kumpatia kandarasi mpya beki wa Ufaransa Aymeric Laporte, 24, kandarasi mpya kutokana na mchezo wake mzuri msimu huu. (Times – subscription requiredManchester United bado wana matumaini ya kuafikia mkataba kuhusu kandarasi mpya ya kipa wa Uhispania David de Gea, lakini kuna wasiwasi kwamba ada ya ajenti inapandisha bei yake. (ESPN)Aliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alikutana na rais wa Paris St-Germain Nasser al-Khelaifi katika mashindano ya tenisi ya WTA mjini Doha wiki iliopita, huku kukiwa na uvumi kwamba mabingwa hao wa Ufaransa hawafurahii kazi ya nkurugenzi wa michezo Antero Henrique. (L’Equipe)

Arsenal wanamchunguza kipa wa Burnley Nick Pope, 26, huku wakitafuta kipa wa kuchukua mahala pake Petr Cech,36 ambaye atastaafu mwisho wa msimu huu. (Mail)Mshambuliaji wa PSG Angel di Maria anasema kuwa uhusiano wake na mkufunzi wa zamani wa Manchester United manager Louis van Gaal ulidorora baada ya kuhoji mbinu yake ya kuwa na usimamizi mkali katika uwanja wa Old Trafford. (Manchester Evening News)

Barcelona wametuma maskauti kumchunguza mshambuliaji wa Ivory Coast na Lille Nicolas Pepe, 23, mshambuliaji wa Ureno,19, Rafael Leao. (France Football)Tottenham wamejiunga na orodha ya vilabu vinavyomchunguza shambuliaji wa Birmingham Che Adams 22. (Birmingham Mail)

Real Madrid wanakaribia kukamilisha mkataba wa kumsajili beki wa Brazil Eder Militao kutoka klabu ya Ureno Porto. (Marca)

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply