BURUDANI

R.Kelly Awa Lulu ujerumani ,Kupiga Naye Picha Tu Uwe Na Laki 8

on

Baada ya lile sakata la unyanyasaji wa kingono lilokuwa likimuandama mkongwe wa muziki R.Kelly na hadi kumpelekea kufutiwa baadhi ya nyimbo alizoshirikiana na wasanii wenzake kwenye mitandao ya muziki, sasa nchi ya Ujerumani imemtaka akatumbuize.

Mwezi April,2019 inaelezwa kuwa R.Kelly anatarajia kutumbuiza mjini Ludwigsburg nchini Ujerumani  katika uwanja wa MHP Arena unaoingiza watu 7,200 ila kutokana na ongezeko kubwa la watu wengi kununua tiketi tamasha hilo litafanyika katika uwanja unaobeba watu 9,000 uliopo nje kidogo ya mji wa Ludwigsburg.

Inaelezwa kuwa kiasi anachotakiwa kulipa shabiki ili  kupata nafasi ya kukutana na kusalimiana na R.Kelly itambidi kulipa Dollar 355 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya shillingi laki nane za Kitanzani huku kiingilio kikitajwa kufikia thamani  zaidi ya laki mbili za Kitanzania kwa mtazamaji wa kawaida.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

1 Comment

  1. bonham

    April 7, 2019 at 9:26 am

    I еvery time spent my haⅼf an һour to read this bⅼog’s content
    everyday along with a cup of coffeе.