HABARI ZA MASTAR

BET Wamwangukia Nicki Minaj!

on

Kupitia mtandao wa twitter wa kituo cha televisheni cha BET nchini Marekani kilionekana kurusha dongo kwa Nicki Minaj baada ya Cardi B kuondoka na tuzo ya Album bora ya Hip Hop(Invasion of Privacy) katika tuzo za Grammy na kauli hiyo ilimfanya Nickikuchukua maamuzi hayo ikiwa pamoja na Lil Wayne ambaye alitajwa kutumbuiza kwenye tuzo za BET June,2019.

“Wakati huu Nicki Minaj amevuta na wigi lake” >>>BET “Young Money haitoshiriki tena katika onyesho la BET Experience wala tuzo” >>>Nicki Minaj 

Baada ya muda mfupi BET wameamua kumuomba msamaha Nicki Minaj kutokana na kauli yao walioitoa dhidi yake na kusema kuwa wanampenda na wamechukua hatua ya kuifuta tweet hiyo na wako tayari kwa lolote ili kuliweka tukio hilo sawa.

Rapper Nicki Minaj ameahidi kuongea kila kitu kuhusu kushindwa kwake kupata tuzo kupitia Radio yake ya Queen Radio na kusisitiza kuwa mashabiki wanatakiwa kujua ukweli na pia Nicki alimaliza kwa kuwapongeza wale wote walioshinda tuzo za Grammy.

EXTR NEWS: ILEJE WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUPATIWA MASHINE YA X-RAY

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply