KITAIFA

Mbunge Wa CHADEMA Hapata Ajari Mbaya Eneo La Dumila

on

Mbunge wa CHADEMA (VM) Bi. Zainab Mussa Hapata ajali eneo la Dumila akitoka Dodoma leo. Abiria wote 3 na dereva wamejeruhiwa. Wametibiwa kwa dharura Morogoro sasa wanapelekwa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi, matibabu zaidi

Bi. Zainab Mussa amepata ajali ya gari eneo la Dumila mkoani Morogoro wakati akitoka jijini Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema- Zanzibar, Salum Mwalimu akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Februari 10, 2019 amesema mbunge huyo alikuwa njiani kurudi nyumbani kwake Pemba visiwani Zanzibar.

Pia, amesema mbunge huyo alipaswa kuhudhuria kikao cha kamati kuu ya chama hicho kinachofanyika leo Jumapili.

“Ni kweli amepata ajali, japo hatujapata taarifa za kitabibu zaidi ila ameumia katika eneo la kifua na alipatiwa huduma ya kwanza katika Hospitali ya Dumila baadaye akapelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na sasa wapo katika utaratibu ili wawalete Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),” amesema Mwalimu.

Mbali na mbunge huyo, abiria wengine waliokuwamo katika gari hiyo pamoja na dereva wamepatiwa huduma ya kwanza na watapelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

5 Comments

 1. check this

  April 8, 2019 at 2:14 am

  It works really well for me

 2. review

  April 24, 2019 at 10:05 pm

  It works really well for me

 3. Young

  April 25, 2019 at 12:46 am

  I enjoy the article

 4. Darell

  April 25, 2019 at 12:50 am

  Thank you for the great article

 5. Eunice

  April 25, 2019 at 2:19 am

  I like the report