HABARI ZA MASTAR

Ommy Dimpoz Ashangazwa Na Maneno Ya Steve Nyerere

on

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa ameshangazwa na maneno ambayo Msanii Steve Nyerere alisema Juu yake.

Akizungumza Kwenye mahojiano aliyofanya siku za nyuma na chombo kimoja cha habari, Steve Nyerere aliibuka na kusema Dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya hali ya ugonjwa wake, huku akiwaomba Watanzania kumuombea na kuwa naye karibu ili apate faraja na kupona.

Ommy Dimpoz amemjia juu Stevw Nyerere juu ya kauli hiyo na kumtaka awe makini na maneno yake kwani hajawahi hata siku moja kumpigia simu na kumjulia hali hivyo asingeweza kujua afya yake.

“Muda mwingine tunapaswa tuzitumie vizuri hizi kamera, kama kuna kitu huna uhakika ni vizuri usikizungumze, ungeweza hata kunitafuta kwanza, ila mimi sina tatizo nae, alijikwaa tu”.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you