HABARI ZA MASTAR

Baada Ya Kupitia Magumu:R.Kelly Atangaza Kufanya Ziara Nchi Za Ulaya

on

    Ikiwa alipitia wakati mgumu sana katika majuma kadhaa nyuma kuhusiana na unyanyasaji wa kingono, Nguli wa R&B duniani R. Kelly ameamua kutangaza balaa barani Ulaya akitarajia kufanya tour katika nchi tofauti barani Ulaya.

Jana aliamua kuchukua jukumu hilo kupitia mitandao ya kijamii na kueleza mpango wake wa tour ya muziki katika nchi ya Australia, New Zealand, na Sri Lanka, pia amepanga kufanya show nchini Ujerumani mwezi Aprili.

 Mipango hiyo imekuja baada ya mwimbaji huyo kukataa mashtaka yanayomkabili dhidi yake na kwamba hakuwa na hatia ya uhalifu wowote wa ngono, licha ya documentary “Surviving R. Kelly” iliyodondoka mtaani ikionyesha namna jamaa alivyokuwa anafanya unyanyasaji wa kijinsia, kimwili na kiakili kwa wasichana wenye umri wa chini ya 18.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you