KITAIFA

Mke Mkubwa Wa Mufti Wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Kuzikwa Leo Korogwe

on

Mke mkubwa wa mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir atazikwa Alhamisi huko kijijini Kwandolwa wilayani Korogwe mkoani Tanga

Marehemu Hidaya Omari Magogo (Mama Shafii) amefariki usiku wa kuamkia leo hospitali ya Kwamndolwa alipopelekwa baada ya kuugua Ghafla usiku wa kuamkia leo Jumatano.

Katibu mkuu wa BAKWATA mwalimu Nuhu Mruma amesema marehemu alikuwa mzima wa afya mpaka ilipofika saa tatu usiku wa jana Jumanne.

Muda huo alianza kuumwa na kupelekwa Hospitali na saa saba kasorobo usiku akafariki Dunia.

Bwana Nuhu Mruma amesema Mufti anatarajiwa kuondoka mapema leo Jumatano kuelekea Korogwe kwa mazishi.

Naye katibu w BAKWATA mkoa wa Tanga Alhaj Riami amesema muda mfupi ujao anatarajiwa kufika KIjijini Kwandolwa kuandaa utaratibu wa Mazishi.

Akiongea kwa njia ya simu na Mwandishi maalum wa mufti akiwa njiani kuelekea kijijini Kwamndolwa alhaj Riami amesema akiwa huko atahakikisha kila jambo linakwenda vizuri ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya wageni wengi wa BAKWATA na Serikali pamoja na taasisi mbalimbali wanaotarajiwa kutoka mikoani.

Naye katibu kiongozi ambaye pia ni katibu wa mkoa wa Singida Alhaj Burhan amemwambia mwandishi wa Mufti kwamba huu ni msiba wa waislamu na watanzania kwa ujumla.

Akiongea kutoka Singida kwa niaba ya makatibu wa BAKWATA mikoa amesema viongozi wa mikoa yote wanatarajiwa kufika Kwamndolwa kushiriki mazishi ya marehemu huyo ambaye amemuita “Mama na mlezi mwema wa waislamu nchini”

Mahmoud Zubeir (mtoto wa mufti) ambaye sasa yupo huko Kijijini Kwamndolwa (km 11 kutoka mjini Korogwe barabara ya Old Korogwe) amesema kwa sasa kinachoendelea kijijini hapo ni matayarisho ya kawaida kupokea wageni.

Akiongea kwa niaba ya masheikh wa mikoa sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Alhadi Musa Salim ameuelezea msiba huo kuwa umewagusa masheikh wote wa mikoa, wilaya na kata kote nchini.

Amesema anafanya utaratibu kuandaa usafiri maalum kwa ajili ya wapenzi wa mufti wa mkoa wa Dar es salaam.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply