MICHEZO

Neymar JR Kuikosa Manchestar United UEFA

on

Miamba ya soka nchini Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain alimaarufu PSG, imethibitisha kuwa mshambuliaji wake raia wa Brazil, Neymar kutokana na kupata majeraha kwenye kifundo cha mguu ule ule ambao aliwahi kuumia na kumkosesha raha kwenye michuano ya kombe la Dunia mwaka jana nchini Urusi, atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki 10.Kuumia kwa nyota huyo kulizua hofu miongoni mwa wapenzi wa soka kuwa huwenda akaukosa mchezo wake wa Champions League dhidi ya Manchester United mwezi ujao., lakini kwa taarifa hizi sasa ataikosa michezo yote miwili dhidi ya miamba hiyo ya Uingereza ambaye michezo yake inatarajia kuanza mwezi wa pili tarehe 12 katika uwanja wa Old Trafford.

Mchezaji huyo ghali zaidi duniani aliumia kwenye mchezo wa French Cup dhidi ya timu ya Strasbourg ambapo waliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply