HABARI ZA MASTAR

Barakah The Prince Mbaroni Kwa Tuhuma Za Utapeli

on

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amedaiwa kuelekeza chini ya ulinzi siku ya Leo kwa kile kinachotajwa ni utapeli ambao Msanii ameufanya.

Siku ya jana kuna video ilisambaa kwenye Mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Barakah akiwa anabishana na maaskari ambao walikuwa wanamkamata na mara moja ilisemekana aliwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituoni.

Stori za chini ya kapeti zinadai kuwa Barakah aliokuwa polisi Baada ya kudaiwa kufanya utapeli ambapo inadaiwa alimtapeli mdada mmoja kiasi Chan shilingi milioni tano kwa ahadi ya kumpa Penzi Lakini Baraka aliishia kuchukua pesa hiyo na kununua gari.

Ulipofika muda wa kumpa Penzi mdada Yule ambaye alikuwa amemzimikia msanii huyo alimpa taarifa kuwa yeye hawezi kuwa naye kimapenzi kwa kuwa yupo na Mpenzi Wake Naj, taarifa hizo zilimvuruga mdada huyo ambaye alihisi ametapeliwa kwani aliishia kumuitia polisi ambao walimtia Ndani.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply