KIMATAIFA

Jumla Ya Watu 19 Wamefariki Katika Shambulio La Kanisa Katoliki

on

Watu 19 waripotiwa kufariki na wengine 48 kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na mabomu mawili yaliolenga kanisa moja ya kikatoliki kaika eneo la Jolo. Tukio hilo limetokea Kusini mwa Ufilipino na kupelekea maafa hayo.

Kulingana na  taarifa iliotolewa na  kamanda wa jeshi la Polisi  Oscar Albayalde, kanisa moja  la kikatoliki limeshambuliwi kwa mabomu mawili  kwa  nyakati tofauti.

Shmbulizi hilo limetokea wakati ambapo kulikuwa kukiendeshwa idadi ya Jumapili katika kanisa hilo.

Delfin Lorenzana, waziri wa ulinzi wa Ufilipino amesema kuwa tayari usalama unaimarishwa katika eneo la tukio huku majeruhi wote wakiwa wamekwishapelekwa kupatiwa matibabu katika hospitali zzinazopatikana karipo na eneo la tukio.

 

EXTR NEWS:TAKUKURU WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA MATUKIO YA MKOANI SONGWE

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply