ELIMU

ELIMU HURU:Haya Hapa Mayai Yanayotibu Saratani!

on

Wanasayansi wamefanikiwa kukuza kuku ambao watakuwa wakitaga mayai yenye uwezo wa kutibu ugonjwa wa kansa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Dr. Lissa Herron na timu yake kutoka chuo cha teknolojia cha Roslin cha mjini Edinburg nchini Scotland, wamefanikiwa kuchanganya kinasaba cha binadamu kinachotengeneza protein katika sehemu ya DNA ya kuku inayohusika na kutengeneza ute mweupe wa yai.

Mayai hayo yatakayozalishwa kutoka kuku hao yatakuwa na uwezo wa kuimarisha mfumo wa ulinzi wa binadamu na kutibu magonjwa kama kansa.

Utengenezaji wa dawa kwa njia hii utashusha gharama ya kutengeneza dawa hizo hadi mara 100 ukilinganisha na uzalishaji wa dawa hizo viwandani.

Herron alisema mchakato huo hautaathiri afya ya kuku kwa aina yeyote ile. Dozi moja ya dawa hio itakuwa sawa na mayai matatu yaliyotagwa na kuku hao.

Kwa mujibu wa watafiti hao ili mayai hayo yaweze kutumika kwa tiba ya binadamu inabidi ipatikane ruhusa ya kisheria, Ruhusa hio ya kisheria inaweza kuchukua kati ya miaka 10 hadi 20 kutolewa.

Matokeo ya Utafiti huo yamechapishwa katika jarida la “BMC Biotechnology”.

EXTR NEWS:IFAHAMU NDEGE KUBWA ZAIDI HAPA DUNIANI YAPEWA KIBALI CHA MATENGENEZO

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply