KIMATAIFA

Rais Wa Sudan Omar al-Bashir Azuru Nchini Misri

on

Rais wa Sudan Omar al-Bahsir amesema kuna jitihada za makusudi zinazofanyika ili kuiiangusha serikali yake kwa kisingizio cha mapinduzi ya kiarabu.

Bashir ametoa kauli hii akiwa ziarani jijini Cairo nchini Misri baada ya kukutana na mwenyeji wake Abdel Fattah al-Sisi. Rais wa Sudan Omar al-Bashir amefanya ziara ya saa moja Jumapili (Januari 27) nchini Misri, ambapo alipokelewa na mwenyeji wake, Abdel Fattah al-Sisi.

Baada ya Qatar, Misri ni nchi ya pili ambayo Rais Bashir anazuru tangu kuzuka wa maandamano yaliyosababisha vifo vya watu 27 kwa mijubu wa serikali ya Sudan, zaidi ya 40 kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Amnesty International.

Maandamano hayo ambayo awali yalikuwa ya kupinga bei ya mkate ambayo iliongezwa maradufu yalibadili mwelekeo na kuwa maandamano dhidi ya rais Omar al-Bashir, huku waandamanaji wakimtaka ajiuzulu.

Nchi nyingi za Kiarabu hazkutia saini kwenye mikataba ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ambayo imetoa hati mbili za kukamatwa dhidi ya rais wa Sudan kwa “uhalifu dhidi ya binadamu” na “mauaji ya kimbari” katika jimbo la Darfur.

Bashir anashtumu “vyombo vya habari” kwamba vinachochea maandamano na kukuza habari za uongo kuhusu maandamano hayo yanayoendelea nchini Sudan. Waandamanaji nchini Sudan wameendeleza maandamano kumtaka kiongozi huyo ambaye ameongoza taifa hilo kwa miaka 30, kuondoka madarakani. Kwa mujibu wa wadadisi Bashri anatafuta uungaji mkono kutoka nchi za Kiarabu na zile za ukanda.

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply