HABARI ZA MASTAR

Msanii Tyga Kutoka Marekani Ataka Milioni 300.7 Kufanya Kolabo Na Daimond Platnumz.

on

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini na CEO wa Music Label ya WCB, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka na kuanika mkwanja mrefu aliotaka Msanii Tuga kwajili ya kolabo naye.

Diamond Platnumz ameanika gharama za kufanya kazi na rapa mkubwa wa Marekani wa lebo ya Young Money, Micheal Ray Stevenson,  maarufu kama ‘Tyga’.

Diamond alifunguka hayo kwenye  mkutano baina ya wasanii na Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) ambao ulihusu suala la asilimia ya malipo kwenye nyimbo za wasanii, Diamond alisema alitaka kufanya kolabo na mwanamuziki  Tyga ambaye alitaka  Dola 150,000 (Tsh.Milioni 300.7).Rapa Tyga anatoka katika lebo kubwa nchini Marekani inayomilikiwa na Lil Wayne, ‘Young Money’. Lebo nyingine ni Last Kings Records, Def Jam Records, Republic Records, Empire Distribution, Cash Money, Universal Motown Records, Decaydance na Good Music.

Diamond ameshafanya kolabo kadhaa na wasanii wakubwa kutoka nje ya nchi ikiwemo Rick Ross na Hivi karibuni Omarion.

TOA MAONI YAKO HAPA