HABARI ZA MASTAR

Monalisa Aomba Msama Kwa Niaba Ya Mwanae Sonia.

on

Mwanadada monalisa amefunguka mbele ya waandishi wa habari na kuwaomba msamha watanzania wote kwa ajili ya mtoto wake wa kike sonia amabe alihojiwa na vyombo vya habari kutokana na ufaulu wake huku akimuongelea mtoto wa kajala ambae pia alikuwa akisoma ane shule moja lakini inavyosemekana ni kuwa hakufaulu vizuri kama mwenzake.

Mtoto huyo alisema kuwa wamekuwa wakisoma wote na muda mwingi amekuwakuwa akitumia kumfundisha lakini kitu kikubwa kajala alikuwa akiongea kukipenda ni fashion na mitindo hivyo anaminikuwa akili yake ipo katika kufanya hivyo.

Hata hivyo watu katika mitandao walimshambulia sana mtoto wa Kajala na kumuita hana akili bila kujua kuwa kufaulu au kufeli kunatokana na sababu tofauti tofauti.

Hata hivyo, monalisa alichukua nafasi hiyo kuomba jamii msamaha kwa kile alichokisema mtoto wake kwakuwa akimetasfiriwa vibaya na watu hata kufikia hatua ya kuwalinganisha jambo ambalo sio sawa.

Monalisa anasema ‘jamani naomba radhi kama kauli yangu kwa mtoto wa kajala  paula imetasfiriwa vibaya , hakukuwa na nia mbaya na hata wakati anazungumza nilikuwepo na wala sikuona ubaya.”

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply