KITAIFA

Wilaya Ya Magu Yang’ara Utoaji Wa Huduma Bora Ya Afya 2018

on

Kituo cha afya Kahangara  kilichoko katika halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza kimeshika nafasi ya tatu kitaifa katika utoaji wa huduma bora za afya na kikiwa kinara katika Mkoa wa Mwanza. Kituo cha afya cha Kahangara ambacho kilikarabatiwa  mwaka 2017, na kukaguliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Majaliwa Kassim Majaliwa  hapo Februari 18, 2018.
Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Magu, Lutengano Mwalwiba amepongeza ari ya watumishi wa kada ya afya na mtazamo wao chanya katika utoaji wa huduma katika vituo  vya afya na zahanati, aidha Lutengano Mwalwiba amesema kuwa mwaka 2018, tumeshika nafasi ya tatu kitaifa tukitanguliwa na vituo vya Katavi na Sirari, Lakini pia kituo  hiki kimezungukwa na zahanati  za Bugabu,John Mongela,Mwamanga,Kinango na Ijinga hivyo kinahudumia takribani wakazi 20540. Wito wangu kwa watumishi wote wajitume kazini bila kulazimishwa na hii ndiyo matokeo chanya kama yaliyopatikana  Kahangara ni juhudi za makusudi.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Magu Dr.Maduhu Nindwa amefafanua vigezo ambavyo hutumiwa na wizara ya afya katika kupima utoaji wa huduma bora, baadhi ya vigezo ni Ubora wa miundombinu iliyojengwa inayopelekea upatikanaji wa huduma bora, Vifaa tiba,uendeshaji wa ukarabati kituo uliofanyika kwa ubora na viwango vinavyokidhi, Kuwahi kuyatumia majengo baada ya ukarabati kwa wakati, Ushirikiano wa watumishi wote wa kituo cha afya kahangara na ari yao ya utoaji huduma kwa kufuata maadili na kuwajali wateja kwa mujibu wa kanuni za kitabibu.
EXTR NEWS: MCHUNGAJI ALIYESHANGAZA UMMA KWA KUSIFIA BANGI

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply