HABARI ZA MASTAR

G Habash Afunguka Na Kusema ” mimi sijawahi sijawahi kumsahau Lady Jaydee”

on

Mtangazaji wa Clouds Fm Gadner G Habash amefungukia tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa amerudiana na aliyekuwa mke wake  Lady Jay Dee.

Siku chache zilizopita Gadner aliposti picha ya kitambo kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mwanamuziki huyo nchini Kenya kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kisima. Katika tuzo hizo za miaka hiyo, Jide alitwaa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike wa Afrika Mashariki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Gardner alisema kuwa anashangaa kwa nini watu waliona ni kitu cha ajabu kwa sababu ni ukweli ulio wazi kwamba hajawahi kuacha kumkumbuka wala hajawahi kumsahau mtalaka wake huyo.

Labda niseme wazi kwamba mimi sijawahi sijawahi kumsahau Lady Jaydee, ndiyo maana mtu akiniambia nimemkumbuka, nashangaa kwa sababu mtu unayemkumbuka ni yule uliyemsahau. Lakini kwangu yeye (Jide) sijamsahau hata kidogo, yupo tu siku zote kwenye akili yangu”.Gadner alipoulizwa kama kuposti picha huko kunaashiria dalili za kurudiana na kurejesha ndoa yao upya, Gardner alicheka mno na kusema alifurahishwa na jambo hilo, lakini kwa sasa angeomba liachwe hivyohivyo.

Hilo la kurudiana? Kwa kweli naomba tuliache kwanza, tuliache hivyohivyo tu”.

Gardner na Jide walifunga ndoa Mei 14, 2005, lakini hawakubarikiwa kupata mtoto. Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka Agosti, 2014.

TOA MAONI YAKO HAPA