MICHEZO

CAF Yatangaza Mabadiliko Ya Tarehe Za Mashindano Kombe La Mataifa Huru Afrika

on

Chama cha mpira wa miguu Afrika (CAF) kimetangaza mabadiliko ya tarehe ya za mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika 2019 litakalofanyika nchini Misri. Mashindano hayo ambayo yalıkuwa yaanze Juni 15 yamesogezwa mbele mpaka Juni 21.

Kwa mujibu wa taarıfa iliyotolewa na CAF mabadiliko hayo yanakuja baada ya maombi yaliyowasilishwa na vyama vya mpıra wa miguu vya Morroco, Tunisia, na Algeria. Baada ya kamati ya dharura kukutana mjini Cairo na kujadili maombi ndipo maamuzi hayo yalipofikiwa. 

Mwaka huu mwezi wa mfungo wa Ramadhani unatarajiwa kuwa baina ya Mei 6 na Juni 3. İli kutoa muda zaidi wa mapumziko kwa wachezaji baada ya mfungo michuano hıyo iliyopangwa kufanyıka baina ya Juni 15 na Julaı 13 sasa imeamuliwa ifanyike baina ya Juni 21 na Julai 19.

Michuano ya kombe hilo miaka iliyopita ilikuwa inasharikisha timu 16 na ilikuwa ikichezwa baina ya Januari na Februari, Mwaka 2019 michuano hio itashirikisha timu 24.

EXTR NEWS: HAYA HAPA MAGOLI WALIYOFUNGWA SIMBA DHIDI YA AS VITA

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply