MICHEZO

Cristiano Ronaldo Azidi Kuinoa Juventus, Sasa Yakaa Kileleni

on

Goli la dakika ya 88 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Cristiano Ronaldo umeifanya Juventus kujisimika kileleni kwa tofauti ya alama 11.

Mchezo huo ulianza kwa Lazio kuwatangulia Juve katika dakika 59, Juve wakasawazisha kupitia Canselo dakika ya 74 na Ronaldo kupiga msumari wa pili na wa ushindi dakika mbili kabla ya mchezo.

Ronaldo alisajiliwa kwa dau la pauni milioni 99.2 mwaka jana, na tayari ameshaifungia Juventus magoli 17.

Mechi hiyo ilionekana kama Juve wataipoteza, na ingekuwa kipigo cha kwanza msimu huu kwa miamba hiyo.

Timu hiyo inayonolewa na Massimiliano Allegri sasa inaonekana dhahiri kunusa ubingwa wa Serie A kwa mara nane mfululizo baada ya timu inayowafukuzia ya Napoli kutoka sare na AC Milan.

EXTR NEWS: HAJI MANARA , MSEMAJI MKUU WA SIMBA ANENA BAADA YA KUFUNGWA 5 BILA

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply