MICHEZO

Wambura Atua Fifa

on

HAKIKA Michael Wambura hataki utani, licha ya kufungiwa maisha na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), habari iliyopo mezani ni kuwa kupitia wakili wake, Emmanuel Muga, amesema kuwa wanaiandikia barua Fifa kuhusu upotoshaji ambao umefanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Juzi Jumatano, Fifa ilitoa taarifa rasmi kuhusiana na kufungiwa maisha aliyekuwa makamu wa rais wa TTF, Wambura ambaye awali alifungiwa hapa nchini mapema Machi, mwaka jana.
Hata hivyo, baadaye Wambura aliamua kupinga uamuzi ambao ulitolewa na kamati ya maadili chini ya mwenyekiti wake marehemu Hamidu Mbwezeleni na kwenda mahakamani.
Novemba 30, mwaka jana, Mahaka­ma Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji Benhaji Masoud walimrejesha kiongozi huyo madarakani baada ya Wambura kuomba mahakama ipitie upya maamuzi ya kamati ya maadili iliyotangaza kumfungia.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Wakili Muga alisema: “Barua ya Fifa, Wambura kufungiwa tumeipokea lakini hii imetokana na upotoshaji ambao ulifanywa na TFF, ndiyo maana maamuzi yakaja kama hayo, hivyo sisi kwa upande wetu tunaandika barua kupeleka Fifa na kuweza kutolea ufa­fanuzi.

“Sababu yale mapitio ambayo yali­tolewa na mahakama kuhusiana na kamati ya maadili naona hayakufika sehemu husika.”

 

 

TOA MAONI YAKO HAPA