MICHEZO

Unai Emery Akubali Manchestar United Ya Ole Gunner Solskjaer.

on

Kocha wa klabu ya Arsena, Unai Emry ameonekana kuihofia Manchester United kwakusema imekuwa hatari huku akidai ni timu nyingine kabisa toka ichukuliwe na meneja Ole Gunner Solskjaer.

Kwa mujibu wa mtandao wa Evening Standard, Arsenal ilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye dimba la Old Trafford mwezi uliyopita ikiwa ni moja kati ya mechi ya mwisho ya aliyekuwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kabla nafasi yake kurithiwa na Solskjaer.

Miamba hiyo ya soka nchini Uingereza itakutana tena usiku wa Ijumaa hii kwenye mzunguko wanne wa michuano ya FA Cup huku kocha mpya wa United, Solskjaer akifanikiwa kupata ushindi kwenye michezo yake yote sabatoka aliporithi mikoba ya Mourinho.

“Ni timu nyingine kabisa, yenye wachezaji wale wale lakini wanacheza katika kiwango cha hali ya juu sasa,’’ amesema Emry huku akiongeza.

 Unai Emry ameongeza ‘’Nimekuwa nikiwatazama katika michezo yao, kila mchezaji anajiamini na kuonyesha kiwango bora kabisa na kwa sasa wamekuwa hatari sana.’’

“Kwa upande wangu ni vizuru kwasababu ni mtihani mzuri kwetu kwenye mashindano haya. Manchester United na sisi tumeshacheza fainali ya FA Cup mara 20 na tumeshinda mara 13 na wao mara 12. Kwa michuano hii ni itakuwa mechi nzuri.’’

“Tunaangalia mbele zaidi kwenye mchezo wetu wa Ijumaa kwa sababu tutakuwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Emirates, ambapo tutakuwa tumezungukwa na mashabiki wengi.’’

Hata hivyo klabu ya Arsenal inasumbuliwa na majeraha ya wachezaji kama vile Hector Bellerin ambaye ameungana na Rob Holding na Danny Welbeck.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

1 Comment

  1. this content

    April 10, 2019 at 3:32 am

    It’s an awesome paragraph in support of all the online viewers; they
    will get advantage from it I am sure.

Leave a Reply