HABARI ZA MASTAR

Rapper DMX Achiwa Huru, Kutoka Jela.

on

Rapper Earl Simmons maarufu kama DMXataachiwa huru kutoka jela hii ni baada ya kumaliza kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukwepa kodi.

Tokea January 2018 DMX alikuwa akitumikia kifungo hicho kwa makosa ya kukwepa kodi kuanzia mwaka 2010 hadi 2016 ambapo alikuwa akidaiwa Shilingi Bilioni 4 za Kitanzania na inaripotiwa kuwa DMX atakuwa chini ya uangalizi wa Mahakama kwa miaka mitatu.Inaelezwa kuwa Ofisi ya shirikisho ya Magereza (Federal Bureau Of Prisons) huachia huru wafungwa siku moja au mbili kabla ya adhabu yao kumalizika ikitokea tarehe yake ya kuachiwa huru au kumaliza kifungo itaangukia weekend ambapo huwa hawafanyi kazi kwa kawaida ni siku ya mapumziko.

TOA MAONI YAKO HAPA