MICHEZO

Jose Mourinho : Ataja Nani Mkali Kati Ya Messi na Ronaldo

on

Siku zote kumekuwa na mdahalo kuwa ni yupi mchezaji bora zaidi ya mwengine kati ya wafalme hawa wawili wasoka duniani Lionel Messi na Cristiano Ronaldo swala ambalo kocha mwenye maneno mengi zaidi Jose Mourinho ametoa mtazamo wake kuhusiana na vita hiyo.

Kocha huyo raia wa Ureno alikutana na swali hilo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na channeli ya ‘beIN SPORTS’ huku akitoa jibu la kisiasa zaidi.

“Messi vs Ronaldo” ni mdahalo wa muda mrefu na nafikiria siyo sawa kuwashindanisha nyota hawa wawili,’’ amesema Mourinho.

Jose Mourrinho ameongeza “Nafikiria siyo sawa kusema mmoja ni bora zaidi ya mwengine kwa mtazamo wangu naona hawafanani.’’

“Kitu pekee ambacho ninaweza kusema ni kwamba, wakati nikiwa na Ronaldo katika upande wangu nilikuwa mwenye furaha. Na wakati nikienda kukabiliana na Messi nilikuwa nafikiria sana namna gani ya kujaribu kuisaidia timu yangu kupata mafanikio.’’

“Kitu cha kuvutia ni miaka ambayo wamekaa kileleni wakiwa bora tu. Kushinda mara moja inawezekana lakini kushinda na kuendelea kushinda tu ni jambo gumu sana kama mchezaji. Hutokea mara moja na kupotea.’’

“Hawa watu wawili wamekuwa bora kwa zaidi ya miaka 10 na kila kitu ni kuhusu wao tu, yani hadi muda huu wao ndiyo wanaoamua, inatosha sasa ni muda wa kuibuka kwa wengine.’’

Jose Mourinho kwa sasa hana kazi baada ya kutimuliwa na Manchester United tarehe 18 ya mwezi Desemba.

 

TOA MAONI YAKO HAPA