
Darassa amesema kuwa stori hizo zilitengenezwa kwa lengo la kuharibu Brand yake kwani walitaka kujua undani wa ukimya wake.
“Sijui ni nani na sijui alitoa wapi? hizo stori zilikuja kwa lengo la kuja kuniharibu kisaikolojia. Lakini nilikuwa very Positive kuzi-handle,“amesema Darassa .
Darassa amesema kimya chake cha mwaka mmoja kwenye gemu, kilisababishwa na malezi ya mtoto wake na kujiandaa kimuziki zaidi ikiwemo kurekodi ngoma kila siku kwenye studio yake ya nyumbani.
Kwa upande mwingine, Darassa amesema kuwa wakati yupo kimya wimbo pekee uliomvutia zaidi ni wimbo wa Iokote wa Maua Sama .
Darassa amekaa kimya kwa miaka miwili bila kuachia ngoma wala kufanya Interview na Media yoyote hapa Tanzania na nje ya nchi.
Related Articles