BIASHARA

EPZA Yashauri Mikoa Kujenga Maeneo Yatakayo Vutia Wawekezaji.

on

Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) imeishauri mikoa mbalimbali hapa nchini kujenga maeneo rafiki yatakayo kuwa chachu kuvutia wawekezaji wa Viwanda na kufika sera ya serikali ya Uchumi wa Kati kupitia Viwanda.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Afisa Mwandamizi Uhamasishaji Uwekezaji Viwanda Panduka Yonazi katika semina ya siku mbili iliwakutanisha Viongozi wa kutoka Mkoa wa Songwe na EPZA lengo likiwa kuwapatia elimu namna ya kutambua fursa zilizopo katika Mkoa wao na kuandaa maeneo kwa ajili ya uanzishaji Viwanda ili kusaidia kuzalisha Ajira kwa wingi.

Sambamba na hayo amesema mikoa ikihamasika kuanzisha maeneo maalumu ya Viwanda itasaidia kukuza sekta ya kilimo ambayo ndio mzalishaji mkubwa wa malighafi za viwandani pamoja na kuziongezea bidhaa za kilimo thamani kwani hapo awali mazao mengi watu walikuwa wanalima kwa ajili ya matumizi ya nyumbani hivyo kupitia Viwanda wengi watahamasika kuzalisha kwa wingi na pato la nchi litaongezeka .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za mitaa wa Mkoa wa Songwe (ALATI) Erick Ambakyse amesema baada ya kupata mafunzo hayo watateua maeneo katika Mkoa wao kwa àjili ya ujenzi wa Uwekezaji wa Viwanda kutokana na mkoa huo kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao mengi ya nafaka kama Mchele, Choroko pamoja na chumvi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ileje Haji Mnasi ameshukuru EPZA kuwapatia semina hiyo katika kipindi hiki wanapolekea kwenye utengenezaji wa bajeti itasaisia kuona frusa nzuri za uwekezaji ambazo zitawezesha kupiga hatua katika sekta ya Viwanda ukizingatia wilaya yao ndio lango kuu la nchi za kusini mwa Afrika hivyo wadau mbalimbali wanakaribishwa kuwekeza.

EPZA imetoa wito kwa mikoa mingine kujenga miundombinu ya kutosha katika maeneo yao ili kusaidia wawekezaji kuongezeka kwani wengi wanapohitaji eneo kwa ajili ya uwekezaji huulizia kwanza miundombinu kama maji ,umeme,barabara ndipo wajenge Viwanda.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

Leave a Reply