Tangaza hapa

MICHEZO

TFF Yaonya Maswala Ya Kimichezo Kupelekwa Mahakamani,Yaofia Kufutiwa Uenyeji Wa AFCON U17

on

Baraza la wadhamini wa shirikisho la  soka nchini TFF limesema maswala ya kimichezo kupelekwa mahakamani kutasababisha Tanzania kufutiwa uenyeji wa mashindano ya AFCON U17 yanayotarajiwa kufanyika hapa nchini baadae mwaka huu.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ammy Ninje akiwa nchini Misri kwenye semina ya wakurugenzi.
Akizungumza na wanahabari leo Mwenyekiti wa baraza hilo Leodgar Tenga amesema kuwa suala la aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho hilo Michael Wambura kwenda mahakamani  linahitaji kumalizwa mapema kwa kutumia busara ili lisiwe na athari kwenye uandaaji wa michuano hiyo.

”Busara ya watanzania itumike ili kulimaliza mapema kwani hili vinginevyo ni jambo ambalo linaweza kugharimu taifa kwa kufutiwa uenyeji wa AFCON U17 ambayo inaanza mwezi April”, amesema Tenga.

Kwa upande mwingine baraza hilo limeunga mkono jitihada na mafanikio ya shirikisho la  soka nchini TFF ambayo yameipatia heshima nchi licha ya timu ya taifa kusuasua.

Wiki hii shirikisho la soka nchini liliweka wazi barua iliyotumwa na FIFA ya kumfungia Waambura kutojihusisha na maswala ya soka huku likiwaonya wanachama wake kutopelekea maswala ya soka mahakamani kwani ni kinyume na katiba ya TFF, CAF na FIFA.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Recommended for you

1 Comment

 1. net worth of kevin hart

  February 18, 2019 at 7:59 pm

  With havin so much written content do you ever run into any issues of plagorism or copyright violation? My website has a lot of unique content I’ve
  either created myself or outsourced but it
  seems a lot of it is popping it up all over the internet without my agreement.
  Do you know any techniques to help prevent content from being ripped off?
  I’d certainly appreciate it.

 2. Loading...

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *